Soma habari ifuatayo kwa makini na kisha jibu maswali yanayofuata:

Question

Wimbi la kusakama wahamiajikutokanchijirani,hasavijanawenyekazi,limeshikakasikatikamiji mbalimbali nchini Afrika Kusini. Watu arobaini wameripotiwa kuuawa hadi sasa, mamia wamejeruhiwa,baadhiwakiwawamechomwamoto.Vijanawenyemapanga,visu,nondo,nyundona mishale wanawasaka mahamiaji majumbani, ofisini na mitaani.

Ghasia hizo zinatokana na vijana wa Afrikakusinikudaikwambawanakosaajirakwasababunafasi zao zinachukuliwa na wageni na wao kubaki wanazururamitaanibilayakazi.Wimbihilolavurugu na mauaji limeiharibia sifa Afrika Kusini nchi ambayo ilifikia hapo ilipo kwa msaada mkubwa wa hali na mali wa nchi za kusini mwa Afrika. Watu wa AfrikaKusiniwamesahaukwambawakatiwa utawala wa makaburu, nchi jirani ziliwapokea maelfu kwa maelfu ya vijana na wazee wa Afrika Kusini kuwapa hifadhi pamoja na kusaidia mikakati ya mapambano dhidi ya makaburu. Pia vijana wa nchi hizo walikosa nafasi za masomo ya juu kutokana na wakimbizi wa Afrika Kusini kupewa upendeleo katika shule za sekondari na vyuo vikuu vya nchi hizo. Lakini leo hii watu wa nchi hizi wanaonekana si lolote si chochote nchini Afrika ya Kusini.

Hivi sasa vijana wengi wamekosa ajira katika nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Malawi na hata Tanzania kwa vile makampuni ya Afrika ya Kusiniyamechukuamakampunimakubwayanchihizo kama vile viwanda vya bia, mabenki na huajiriwatukutokaAfrikaKusinikufanyakazihuko.Suala hilo limehamasisha kukimbilia Afrika Kusini kwa vijana wengi ili kupata ajira.

Sasa njia pekee iliyobaki kwa vijana wa nchijiraniwasiokuwanakazinikuzifuataajirahizoAfrika Kusini. Wageni, hasa kutoka nchi za Afrika, wamekuwa wakikutana na vikwazo vya kupata vibali vya kufanya kazi, lakini wamekuwa wakitumia njia za panya kupata ajira. Vijana wengi wa Afrika Kusini wamekuwa wakikosa ajira kutokana na elimu ndogo au maambukiziyavirusivyaUKIMWI  yaliyozagaa nchini humu ukilinganisha na nchi jirani.

Takwimu za serikali, kwa mfano, zinaonesha zaidi ya asilimia thelathini (30%) ya wafanyakazi wa kwenyebandariyamjiwaDurbannamaeneoyaukandawaPwani,wanaishinavirusivyaUKIMWI na makampuni ya maeneo hayo yamekuwa yakibagua katika ajira maana uwezo wa watu hao kufanya kazi za sulubu ni mdogo kwa sababu ya UKIMWI.

Kwa ujumla ghasia zimezusha wasiwasi mkubwa kwa Afrika Kusini, nchi ambayo inakabiliwa na maandalizi ya kuwa mwenyeji wa michuano ya fainali za Kombe la Dunia kwa mchezo wa soka mwaka 2010. Inatarajiwa kuvutia wageni wapatao nusu milioni. Wasiwasi unakuja kwa vile kiasi kikubwa cha fedha kimetumika katika maandalizi na faida yake inatarajiwa kupatikana wakati wa mashindano hayo. Hivyo vitendo vya mauaji vinatia doa. Upo uwezekano wa kukosa nafasi hiyo kutokana na kuhofia usalama na amani kwa wanamichezo.

 

Maswali

(a) Kichwa cha habari hii kinachofaa ni kipi?

(b) Vijana wengi kusini mwa Afrika wamemiminika Afrika Kusini ili wapate ajira. Eleza mambo mawili (2)​ yaliyosababisha vijana hao wapate ajira Afrika ya Kusini.

(c) Ungeishauri nini serikali ya Afrika ya Kusini?

(d) Makampuni yanahofia kuwaajiri vijana wa Afrika Kusini. Ipi sababu kubwa ya hofu hiyo?

 

Andika ufupisho wa aya mbili za mwisho za habari uliyoisoma kwa maneno ​hamsini (50)​.

Leave an answer

Sorry, you do not have permission to answer to this question .